18 Juni 2025 - 14:54
Taarifa ya Pamoja ya Nchi 21 za Kiarabu na Kiislamu Kulaani Shambulio la Israel Dhidi ya Iran

Katika taarifa hiyo, nchi hizo zimetilia mkazo umuhimu wa kuondoa silaha za nyuklia na silaha nyingine za maangamizi ya halaiki kutoka katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (as) -ABNA- ikinukuu televisheni ya Al Jazeera ya Qatar, Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi 21 za Kiarabu na Kiislamu wametoa taarifa ya pamoja wakilaani vikali mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.

Katika taarifa hiyo, nchi hizo zimetilia mkazo umuhimu wa kuondoa silaha za nyuklia na silaha nyingine za maangamizi ya halaiki kutoka katika eneo la Mashariki ya Kati.

Pia, nchi hizo zimeonya kuwa kuendelea kwa vitendo vya aina hiyo vya uvamizi kunahatarisha kwa kiwango kikubwa amani na usalama wa kikanda na kimataifa.

Wametaka jumuiya ya kimataifa iheshimu na izingatie misingi ya sheria za kimataifa na Katiba ya Umoja wa Mataifa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha